TUME ya Taifa ya kudhibiti
Ukimwi (Tacaids) inatarajia kuanza kudhibiti maambukizi mapya kwa makundi
mbalimbali ikiwamo wavuvi na madereva ili kufikia malengo ya kimataifa.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa tume hiyo, Yassin Abas.
Akizungumza
katika kikao kazi cha kuendeleza mkakati wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa tume hiyo, Yassin Abas, alisema mpango huo
unalenga kukabiliana na maambukizi mapya kutokana na tabia ya maisha ya watu wa
maeneo hayo.
Alisema
jumla ya Sh milioni 660 zimetengwa kufanikisha mpango huo utakaotekelezwa
katika maeneo ya mwambao wa ziwa Viktoria na visiwa vyake, Ziwa Tanganyika,
migodi ya madini ikiwamo Simanjiro mkoani Manyara na barabara kuu za kutoka Dar
es Salaam kwenda Tunduma, Arusha, Burundi na Rwanda.
Waandishi wa Habari wakiwa katika kikao hicho.
"Katika
kundi hili la madereva tumewalenga madereva wa masafa marefu kutokana na kuwa
miongoni mwa makundi hatari kwa sababu wanasafiri na kuwa mbali na familia zao.
"Na
kwa taarifa yenu wale madereva wana wapenzi katika kila kituo wanachotembea kwa
hiyo wanahama na virusi vya Ukimwi ambao hatimaye huupeleka katika ndoa zao
hivyo kuziweka katika hatari kubwa ya kuambukizwa" alisema Abas.
Alisema hadi
sasa tayari wameanzisha vituo vya maarifa vitakavyosaidia kupunguza maambukizi
kwa madereva ambapo katika vituo hivyo madereva watapewa elimu na msaada
utakaowakinga na maambukizi ikiwamo kuwapatia kondom na ushauri.
Alisema
baadhi ya vituo vilivyojengwa vipo katika maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam,
Ipogolo mkoani Iringa na stendi ya mabasi ya Tunduma, Manyoni mkoani Singida,
Mdaula na Kagongwa.
Akizungumza
katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko, alisema
wanaume wamekuwa kikwazo katika mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kutoka na
idadi kubwa ya wanaume kutafahamu kama wameambukizwa virusi hivyo.
Dk.
Maboko alisema tafiti zinaonesha kuwa watu 52 kati ya 100 wanafahamu kuwa
wameambukizwa virusi vya Ukimwi na kati yao ni asilimia 45 tu ya wanaume
wanaofahamu kuwa wameambukizwa huku wanawake wakiwa ni asilimia 56.
"Hii
inaonesha wanaume wanaofahamu ni 45 tu kati wa 100 na 55 hawajui kuwa
wameambukizwa. Kwa wanawake wao ni 56 wanaofahamu kuwa wameambukizwa na
wasiofahamu ni 44" alisema Dk. Maboko.
Alisema
hadi sasa Tanzania inafanya vizuri kuelekeza malengo ya kimataifa ya kufikia 90
tatu, ambazo ni pamoja na kupima asilimia 90 ya watu walioambukizwa, kuanza
kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi na kufubaza virusi
hivyo.
Aliongeza
kuwa katika tisini ya kwanza na ya pili na ya tatu Tanzania imefikia hatua
bora, kuelekea malengo ya kitaifa na kimataifa ambapo eneo la kuanza matumizi
ya dawa wamevuka malengo ambapo asilimia 91 ya waliopimwa wameanza dawa na kati
yao asilimia 88 wamefanikiwa kufubaza maambukizi.
"Hii
itatusaidia kufikia malengo ya kimataifa la 2030, la kufikia sifuri tatu ambazo
ni pamoja na kutokuwapo kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, kutokuwa na
vifo vitokanavyo na Ukimwi na kuondoa unyanyapaa wa aina zote katika
jamii" aliongeza Dk. Maboko.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS ),Jumanne Issango akitoa mada wakati wa kikao hicho.
Mtoa mada, Charles Kayoka akisisitiza jambo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko, akiendelea kutoa ufafanuzi Mikoa kuongezeka kwa maamukizi mapya ya virus vya
ukimwi.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye majadiliano wakati wa kikao hicho
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko,Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS ),Jumanne Issango (katika) wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakati wa kikao kazi cha kuendeleza mkakati wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
No comments:
Post a Comment