Katibu wa Mashindano
ya Kombe la Mei Mosi, Bw. Award Safari (wa pili kushoto), jana akiongea na
wanamichezo awapo pichani kwenye uwanja wa Samora akitoa maelezo mbalimbali ya
kuhusiani na mashindano hayo, ambayo yameanza jana na ufunguzi utafanyika rasmi
April 21, 2018 .
(Picha na Bahati Mollel-TAA).
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa kamati ya michuano ya Kombe la Mei Mosi katika kikao kilichofanyika jana kwenye uwanja wa Samora, yakiwa ni maandalizi ya michuano hiyo iliyoanza Aprili 16,2018 (Picha na Bahati Mollel-TAA)
Afisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Iringa, Bw. Mweri Kilimali (aliyesimama) akielezea kifungu namba 28 kinachohusiana na ubadhirifu wa mali za serikali kwa wachezaji wanaoshiriki mashindano ya Kombe la Mei Mosi yanayofanyika katika uwanja wa Samora. (Picha na Bahati Mollel-TAA).
Wachezaji wa timu ya Uchukuzi wakisikiliza maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Kamati ya Michuano ya Kombe la Mei Mosi katika kikao kilichofanyika jana kwenye uwanja wa Samora, mkoani Iringa. Michuano hiyo itazinduliwa rasmi Aprili 21, 2018 na Mkuu wa Mkoa Mhe. Amina Masenza.
(Picha na Bahati Mollel-TAA).
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa kamati ya michuano ya Kombe la Mei Mosi katika kikao kilichofanyika jana kwenye uwanja wa Samora, yakiwa ni maandalizi ya michuano hiyo iliyoanza Aprili 16,2018 (Picha na Bahati Mollel-TAA)
Afisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Iringa, Bw. Mweri Kilimali (aliyesimama) akielezea kifungu namba 28 kinachohusiana na ubadhirifu wa mali za serikali kwa wachezaji wanaoshiriki mashindano ya Kombe la Mei Mosi yanayofanyika katika uwanja wa Samora. (Picha na Bahati Mollel-TAA).
Wachezaji wa timu ya Uchukuzi wakisikiliza maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Kamati ya Michuano ya Kombe la Mei Mosi katika kikao kilichofanyika jana kwenye uwanja wa Samora, mkoani Iringa. Michuano hiyo itazinduliwa rasmi Aprili 21, 2018 na Mkuu wa Mkoa Mhe. Amina Masenza.
Na Bahati Mollel-TAA, Iringa
WACHEZAJI
wanaoshiriki kwenye michuano ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea kwenye uwanja wa
Samora mkoani Iringa, wametakiwa kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja,
imeelezwa.
Mjumbe
wa Kamati ya michezo hiyo, Bi. Joyce Benjamin amesisitiza wachezaji wote
kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa kuwa na nidhamu popote wanapokuwa
kwenye mkoa wa Iringa, ikiwemo ya kuvaa mavazi ya staa na kuwa na kauli nzuri
kwa wachezaji wenzao, viongozi na
waamuzi.
Bi.
Bebnjamin amesema haipendezi na haileti sifa nzuri kwa wachezaji hao ambao timu
zao zinatoka kwenye wizara na taasisi za umma kuonesha utovu wa nidhamu, ambapo
watakuwa wamekwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
“Haitapendeza
kumuona mtumishi wa umma ambaye yupo hapa katika michezo amevaa nguo zisizokuwa
na staa, fupi, za kuonesha maungo na za kubana na kuja nazo huku uwanjani au
kutembea mitaani, pia kutoa kauli chafu kwa wachezaji au viongozi wa timu yake
au pinzani au kwa waamuzi, hatutasita kumuandikia barua kali ya karipio na
nakala kupelekwa kwa mwajiri wake ili amchukulie hatua zaidi za kinidhamu,”
amesema Bi. Benjamin.
Nayo
taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), imesema itafanya
ukaguzi wa wachezaji wanaoshiriki kwenye michuano hiyo, ili kubaini wachezaji
wasio waajiriwa wa serikali ‘mamluki’, kwa kuwa sio sheria kutumiwa kwa
wachezaji hao.
Akizungumza
jana na wachezaji waliowasili mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki kwenye
michezo hiyo, Afisa kutoka Takukuru, Bw. Mweri Kilimali amesema endapo
watabaini kuwepo kwa wachezaji hao watawachukulia sheria ikiwemo ya kufunguliwa
kesi ya uhujumu uchumi na kuingizia serikali hasara.
“Hawa
wachezaji wanakuwa wakitumia rasilimali za serikali kwani wanakuwa wamelipiwa
posho kutoka serikalini kutokana na taasisi au wizara iliyomsajili, hivyo wote
waliohusika akiwemo Afisa Utumishi watachukuliwa sheria kutokana na kuihujumu
serikali na watafungwa kutokana na kosa hilo, kwani wanakuwa wamekula njama ya
kumsajili mtu ambaye sio mtumishi wa umma na kumlipa posho kutoka katika fungu
la fedha za serikali,” amesema Bw. Kilimali.
Bw.
Kilimali amewataka viongozi wote wa michezo walioambana na timu zao kuhakikisha
wanawasomea wachezaji kanuni hizo za mashindano na kuweka msisitizo kila wakati
ili wasiende kinyume na kanukni hizo, hivyo wasidhubutu kufanya kosa la kukiuka
na kutumia madaraka yao vibaya na kusajili wachezaji wasiokuwa waajiriwa halali
wa serikali, kwa kuwa ni kosa lililopo chini ya kifungu namba 28 cha makosa ya
ubadhirifu na watafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuwa watakuwa
wameiingizia serikali hasara.
Naye
Katibu Mkuu wa Kamati ya michezo ya Mei Mosi, Bw. Award Safari amesema adhabu
mbalimbali zitatolewa kwa watakaochezesha mamluki kwa mujibu wa kanuni za
michezo hiyo namba 13.0 kipengele 13.1 ambapo kiongozi au viongozi
watakaohusika kumsajili mamluki atafungiwa kwa kipindi cha miaka miwili, huku
mchezaji husika ataondolewa katika kituo cha mashindano, na timu husika
itapigwa faini ya sh. 500,000.
Bw.
Award amesema adhabu nyingine ni timu husika iliyochezesha mamluki
itanyang’anywa ushindi endapo itakuwa imeshinda, huku viongozi au kiongozi
aliyehusika kusajili mamluki ataandikiwa barua na nakala yake itapelekwa kwa
mwajiri wake, ikionesha udanganyifu aliofanya na kuiingizia ofisi yake hasara.
“Ili
kudhibiti mamluki lazima kila mwanamichezo atatakiwa kuwa na kitambulisho chake
halisi cha kazi, kadi ya bima ya afya, kadi ya mfuko wa jamii na hati ya malipo ya mshahara yaani salary
slips za miezi miwili ya Februari na Machi 2018, na vitatumika kama vielelezo
endapo mchezaji yeyote atalalamikiwa kuwa ni mamluki,” amesema Award.
Award
amezitaja kanuni nyingine kuwa ni pamoja na usajili ni lazima wachezaji wote
wajaze fomu maalumu zitakazotolewa na Kamati ya mashindano itakayokuwa na kmajina
na picha yake halali; pia kanuni ya ushindi utatambulika kwa pointi, magoli ya
kufunga na kufungwa, na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na endapo
timu zitafungana kwa kila kitu basi utaratibu wa kurushwa shilingi utatumika.
No comments:
Post a Comment