Dotto Mwaibale na Philemon Mazalla Singida
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida umekamilisha maandalizi ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani ambapo kilele
chake ni Octoba 7, 2022 siku ya Ijumaa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Meneja wa NSSF Mkoa wa
Singida, Oscar Kalimilwa alisema na wao wanaadhimisha siku hiyo kuonesha
kuwajali wateja wao chini ya kauli mbiu isemayo ‘Huduma bora ndio kipaumbele
chetu’
Alisema katika maadhimisho hayo wameandaa baadhi ya shughuli ambazo
watazifanya siku hiyo ya kilele ambapo watachangia damu, kutoa msaada wa vitu
mbalimbali Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa.
Alisema siku hiyo ya kilele wameandaa keki maalumu ambayo itakatwa na
wataila pamoja na wateja wao ikiwa ni ishara ya kuwathamini kwani ndio wanaowafanya
waendelee kuwepo na kuwa wamejipanga vilivyo kuifanya siku hiyo kuwa ya
mafanikio kwao na wanachama wao.
Aidha Kalimilwa alisema wataitumia siku hiyo kutoa elimu kwa wanachama ambao hawana elimu kuhusu mifuko hiyo ya jamii na akatoa wito kwa wananchi na wanachama wao waendelee kuiamini NSSF kwani kuwepo kwake kunasaidia kupambana na majanga yanayomtokea binadamu.
No comments:
Post a Comment