WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amekuwa mbogo baada ya kusikia mbolea bado
hazijaanza kusambazwa kwa wakulima mkoani hapa licha ya msimu wa kilimo kuanza ambapo ameagiza
zoezi la kuzipeleka walipo wakulima kote nchini lianze mara moja.
Bashe ametoa agizo hilo leo Oktoba 5, 2022 wakati akikagua mabanda yenye
pembejeo za kilimo kabla ya kuzindua msimu wa kilimo wa 2022/ 2023 kwa Mkoa wa
Singida ambayo pia aliongoza zoezi la ugawaji wa mbegu za alizeti zenye ruzuku
ya Serikali.
Bashe alisikitika kusikia kuwa wakulima wa Mkoa wa Singida mpaka sawa
hawajui watapata wapi mbolea maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Juma
Killimbah.
" Meh.Waziri kumekuwa na changamotochangamoto kubwa ya namna ya
wakulima wetu kupata mbolea zaidi ya kusikia kwenye vyombo cha habari"
alisem Killimbah.
Kufuatia maelezo hayo Waziri Bashe alimuita Afisa Kilimo wa Manispaa ya
Singida na kumuhoji kuhusu jambo hilo licha ya kupatiwa mafunzo ya mfumo wa
usambaziji wa pembejeo.
"Afisa kilimo baada ya kupewa mafuzo mmeweza kuyatoa kwa wananchi na
madiwani ili mfumo huu wauelewe? Afisa kilimo alijibu hawajayatoa ndipo Waziri
Bashe alikuwa mbogo na kusema mafunzo hayo waliyapata ili iweje kama si
kuwafikishia walengwa".
Bashe alisema kuanza sasa hatapenda kusikia kuna Mkoa wakulima hawajapata
mbolea hivyo aliagiza ipelekwe na kusambazwa maeneo yote na akawataka wakulima
wajisajili kwa ajili ya kununua mbolea hiyo na ambaye hata jisajili hata kuweza kununua.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza wakati akimkaribisha
Waziri Bashe ili kuzindua msimu huo wa Kilimo wa 2022/ 2023 aliipongeza
Serikali chini ya Rais Samia Suluhu
Hassan kwa kuongeza bajeti ya kilimo kutoka Sh.294.1 Bilioni hadi Sh.751.1
Bilioni sawa na ongezeko la asilimia
155.34. bajeti ambayo haijawai kutokea
katika awamu zote za marais waliomtangulia.
Alisema lengo la Rais Samia kuongeza bajeti hiyo ni kuwatoa wananchi katika
umaskini kwa kufanya kilimo cha Sayansi na si vinginevyo.
Alisema Mkoa wa Singida umejipanga kuongeza maeneo ya kilimo ambapo aliwahimiza wananchi kwenda mashambani kulima kwa bidii.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dk.Godfrey Mkamilo alisema katika suala la upatikanaji wa mbegu watashirikiana na ASA na kuhakikisha wanazalisha mbegu la zao la kimkakati la Alizeti.
Dk. Mkamilo pia alisema watasaidia kutoa mafunzo kwa maafisa ugani na wakulima kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa zao la alizeti hapa nchini.
No comments:
Post a Comment