Dotto Mwaibale na Philemon Solomon, Singida
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida umeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kutoa
msaada wa damu, sabuni, mashuka, pampasi mafuta ya kupaka, nguo za watoto, dawa
za meno na miswaki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Akizungumza katika
maadhimisho hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa alisema
wametoa msaada huo kwa jamii kuonesha kuwajali wateja wao na wananchi chini ya
kauli mbiu isemayo ‘Huduma bora ndio kipaumbele chetu’
Alisema mbali na kutoa
msaada huo waliandaa keki maalumu walioila pamoja na wateja wao ikiwa ni ishara
ya kuwathamini kwani ndio wanaowafanya waendelee kuwepo
Aidha Kalimilwa alisema
walitumia siku hiyo kutoa elimu kwa wanachama ambao hawana elimu kuhusu mifuko
huo wa jamii ambao ni muhimu sana na kutoa wito kwa waajiri kuendelea kutoa
michango ya wanachama wao ili wanapokutana na majanga ambayo NSSF inashughulika
nayo kuwahudumia iweze kuwasaidia kwa kutoa huduma bora kama kauli mbiu yao
inavyosema.
Mhasibu wa NSSF Mkoa wa
Singida, Keneth Kalinjumani aliwapongeza wanachama wote walioamua kujiunga NSSF
kwani hawezi kujuta kwani mfuko huo unatoa huduma bora na hawatajuta katika
maisha yao.
Alisema NSSF inafanya vitu
vingi vya kuwasaidia wanachama wao vya kuwakinga na majanga na akawahimiza
waajiri kutosita kuwapeleka waajiriwa waokuwaandikisha katika mfuko huo kwani
watakuwa wakiwawekea mazingira mazuri baada ya kustaafu utumishi wao.
Afisa Huduma kwa Wateja
Latifa Singano aliwahimiza wananchi kujiunga katika mfuko huo ili waweze
kuwahudumia kwani ndio jukumu lao.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Mkoa wa Singida, Lucretia Mseli akipokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo aliwashukuru NSSF kwa kutoa faraja kwa watu wenye uhitaji waliopo hospitalini hapo ambapo alitoaa wito kwa wadau wengine na mtu mmoja na taasisi waguswe kwa kutembelea katika zahanati, hospitali na vituo vya afya kuwaona wagonjwa wenye uhitaji na kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment