Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Hosiptali ya CCBRT, Brenda Msangi akitoa mada yake wakati wa
kongamano la mwanamke kwenye ushawishi kufikia ndoto ya mafanikio kimaendeleo jijini Dar es Salaam.
HABARI PICHA/NA PHILEMON SOLOMON
............................................................
WANAWAKE nchini wametakiwa kujitambua jambo litakalo wasaidia kujiepusha na vitendo vya ngono maofisini.
Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi wakati akitoa mada katika kongamano la mwanamke kwenye ushawishi kufikia ndoto ya mafanikio kimaendeleo lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema masuala ya unyanyasi wa kingono maofisi yapo lakini yanashindwa kuweka hadharani kwa kuwa yanafanyika kisiri na walengwa wakubwa wakiwa ni wanawake.
"Wanawake tunatakiwa kujitambua kuanzia uvaaji wetu, jinsi tunavyozungumza hali hiyo itaondoa dhana ya kuwa sisi wenyewe tunapenda kufanyiwa vitendo hivyo.
Alisema kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono maofisini lakini kupitia kongamano ili tunaweza kupiga hatua ya kukabiliana na changamoto hiyo na ndio maana baadhi ya washiriki, wakurugenzi kutoka katika makampuni.
Msangi alisema kukiwepo na mifumo mizuri maofisini itasaidia kujua namna ya kumsaidia muathirika wa vitendo hivyo na hatua za kuchukua.
"Mwanamke akijengwa kifikra na kuwa na uthubutu anaweza kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.
Mmoja wa wakurugenzi wa shirika hilo, Emelda Mwamanga alisema kwa zaidi ya miaka 10 tangu waanzishe shirika hilo mwaka 2008 wamekuwa wakitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wa kibiashara na kufanya matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuibua vipaji ili kuwainua kiuchumi.
Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la Woman of Influence la jijini Dar es Salaam.
Meneja
Mipango na Usimamizi wa Utendaji Afrika Mashariki kutoka Kampuni TBL,Nancey
Riwa (kushoto) akichangia mada wakati wa
kongamano hilo (katika) Mkurugenzi wa Uhusiano kutoka VodaCom, Rosalynn
Mworsia, na kulia Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hosiptali ya CCBRT, Brenda
Msangi.
Program
Meneja Mwandamizi kutoka Kampuni ya Trade Mark, Monica Hangi (aliyesimama
kushoto) akifurahia jambo wakati akichangia mada.
Kongamano likiendelea.
No comments:
Post a Comment