Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo (AQRB) Yawajengea Uwezo Waandishi wa Habari. - FAHARI NEWS

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, June 30, 2019

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo (AQRB) Yawajengea Uwezo Waandishi wa Habari.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Arch. Dkt Ludigija Bulamile akifungua  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
  Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Arch.Albert Munuo, akisoma taarifa kuhusu majukumu ya bodi hiyo (kulia) Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Ludigija Bulamile.
 Afisa Mkuu wa Sheria Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Ibrahim Mohamed akielezea makosa mbali mbali ya kisheria yanayofanywa yakiwemo yale ya uuzwaji wa ramani hadharani pasipo kufuata taratibu. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Arch . Dkt Ludigija Bulamile akipitia taarifa mbali mbali za bodi hiyo.
 Watumishi wa bodi hiyo wakiwa katika  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
 Afisa Mdhibiti Mwandamizi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Mlezi Makuka (kushoto aliyesimama) akichangia mada yake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
 Arch. Mbaraka Igangula akichangia mada.
 QS.Mashaka Bundara akisisitiza jambo.
  Arch.Joseph Ringo akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
 Waandishi wa Habari wakichangia mada mbali mbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo  yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Dkt. Ludigija Bulamile akijibu maswali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Dkt. Ludigija Bulamile,  Kaimu Msajili  Albert Munuo pamoja na waandishi wa habari na wajumbe wa bodi hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) 
.................................................
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imewataka wanahabari nchini  kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.

Akizungumza alipokuwa akifungua   mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  yaliyoandaliwa na menejimenti ya bodi hiyo mwishoni  mwa wiki Jijini Dar es salaam   Mwenyekiti wa AQRB  Dkt. Ludigija Bulamile alisema lengo ni kuwaelimisha waandishi shughuli na majukumu yake katika sekta ya ujenzi ili waweze kuuelimisha umma wa watanzania faida na hasara za kutowatumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi wanapofanya ujenzi wowote. 

 Alisema kumekuwa na mkanganyiko  wa utoaji taarifa unaofanywa na waandishi wakati wanaripoti masuala yanayohusu  taaluma hizo hivyo  ili kuondoa mkanganyiko huo wanahabari wana kila sababu ya kuyatumia mafunzo haya kwa kuwaelimisha wengine  kuzitumia kalamu zao kuuelimisha umma tofauti za taaluma hizo.

'EIelimisheni jamii  umuhimu wa kuwatumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika ujenzi ili waweze kupata makazi  bora, ambayo pia yatawapa nafuu kwenye gharama za ujenzi kulingana na matakwa,'.alisema Bulamile.  

Aliongeza kufafanua zaidi sababu za wahandisi kufahamika zaidi na umma kuliko wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi pamoja na kufanya kazi zinazoshabihiana kuwa ni pamoja na  taaluma hiyo kuchelewa kuingia  nchini.   

" Mpaka sasa nchi nzima ina   wataalamu wa taaluma hii  wasiozidi 1,500 hili bado ni tatizo kulingana na idadi ya watu na mahitaji yake," alisema Dkt. Bulamile  na kuongeza bodi imeendelea kuongea na baadhi ya vyuo vikuu vilivyopo nchini vione umuhimu wa kufundisha taaluma hii ili kuongeza idadi ya wataalamu watakaowezesha kuibadili sura ya nchi hapo baadae katika sekta ya ujenzi  kwa kubuni majengo ya kisasa yanayoendana na wakati.

 Kwa upande wake Kaimu Msajili wa bodi Mkadiriaji Majenzi Albert Munuo alisema kuwa,pamoja na kusajili wataalamu wa fani hiyo na makampuni pia wanamajukumu ya kukagua miradi ya ujenzi inayoendelea ili kuona kama wataalamu wamehusika.

" Tumekuwa tukikagua ujenzi wa miradi mbalimbali  mikubwa inayoendelea na kwamba kwa sasa tunajipanga kuutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR ili kujionea ni kwa namna gani Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi wameshiriki ,'alisema  Munuo

Aliongeza kuwa AQRB ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi na kwamba mpaka sasa ina ofisi katika kanda tano ikiwepo Kanda ya Mashariki, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini ,nyanda za juu kusini na kanda ya kati. 

Mafunzo hayo pamoja na kuhudhuriwa na baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali zikiwepo televisheni, redio na magazeti pia wataalamu wengine wa ujenzi kutoka AQRB akiwepo mwanasheria wao alishiriki na kusema yapo makosa mbali mbali ya kisheria yamekuwa yakifanywa ikiwepo lile la uuzwaji wa ramani hadharani pasipo kufuata taratibu. 


Hata hivyo wataalamu hao waliongeza kutolea mfano kwa kusema asilimia 90 ya nyumba zilizojengwa Dar es salaam zimejengwa bila vibali na kusababisha hasara kwa jamii pale ambapo eneo hilo linapokuja kubainika kuwa si mahali  sahihi kwa ujenzi wa makazi na kulazimika kubomolewa. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages