Mkurugenzi wa Usalama
na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Julius Chambo akifafanua jambo kwenye hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya
tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara
kwa mafundi sanifu yanayofanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa
mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi
wa barabara wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mafunzo hayo iliyotolewa na
Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo.
Mhitimu wa mafunzo ya
tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa
barabara akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo mara baada
ya kuhitimu mafunzo hayo.
Mwakilishi wa wahitimu
wa mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya
ujenzi wa barabara, Bw. Seth Rengia akiwasilisha maoni ya wahitimu wa mafunzo
hayo kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Usalama
na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Julius Chambo (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi
wa barabara yanayofanyika mkoani Morogoro.
Imetolewa
na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment