WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa mkoa
wa Mwanza kuendelea na usaji wa wanunuzi wa zao la pamba na wawape fursa ya kuchagua maeneo wanayotaka kununua pamba.
Ametoa kauli hiyo
jana jioni (Jumapili, Aprili 02, 2018) alipozungumza na viongozi mkoa wa Mwanza
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
wa Mwanza akiwa njiani kuelekea mkoani Geita.
Waziri Mkuu leo
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha mwenge wa Uhuru
zitakazofanyika mkoani Geita. Kauli mbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni
‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
Waziri Mkuu alisema
wakati viongozi hao wakiendelea na usajili wa wanunuzi wa pamba ni vema wakawapa
nafasi ya kuchagua maeneo watakayohitaji kukunua kwa sababu yanaweza
kurahisishia usafirishaji.
Hata hivyo, Waziri
Mkuu aliwasisitiza viongozi hao kuendelea kusimamia na kufuatilia maendeleo ya
zao hilo kwa umakini zaidi ili kuweza kubaini changamoto zitakazojitokea na
kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.
Alisema kutokana na
mwenendo wa hali ya hewa mwaka huu wakulima wa zao la pamba wanatarajiwa kuvuna
pamba nyingi, hivyo ni vema ukatengenezwa utaratibu utakaomrahisishia mkulima
kutoa mazao shambani na kufikisha mnadani.
Waziri Mkuu alisema
utaratibu huo wa kutoa mazao shambani na kupelekwa mnadani kwa wakati ni muhimu
kwa sababu utasaidia katika kulinda pamba ili isipoteze ubora wake.
Zao la pamba ni
miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali imeamua kuyapa kipaumbe
kwa kuyafuatilia kuazia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, pembejeo
pamoja na uuzaji. Mengine ni korosho, chai, kahawa na tumbaku.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, APRILI 02, 2018.
No comments:
Post a Comment