Ajali ya Basi la Lugano mlima K9 Ngara,Kagera,Yaua Wakimbizi Watano. - FAHARI NEWS

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, March 30, 2018

Ajali ya Basi la Lugano mlima K9 Ngara,Kagera,Yaua Wakimbizi Watano.

 Umati wa Wananchi wa Kijiji cha Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera wakijitahidi kuokoa  Watu waliojeruhiwa  vibaya kufuatia ajali ya Basi moja kati ya Manane yaliyokuwa yakisafirisha Wakimbizi wa Burundi kutoka kambi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma kuelekea nchini Burundi kupinduka leo March 29, 2018  katika  eneo hilo.
 Pichani Basi hilo likiwa limeharibika Vibaya.

Ajali hiyo imetokea saa 10 jioni  katika mteremko  wenye kona kali wa mlima K9 barabara kuu ya Benaco –Ngara  ambapo Basi lilipoteza mfumo wa breki aina ya Higer lenye namba za usajili T 331 DFV ambalo lililigonga kwa nyuma Basi linguine aina ya TATA Star  lenye namba za usajiri T 765  DLD  Mali ya kampuni ya Lugano (Kampuni ya Mtipa Investment ) ya mkoani Kigoma na kusababisha Vifo vya Watu watano papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa. 
 Wananchi wakiendelea kutoa msaada wa kukata miti ili kuokoa Majeruhi .
 Wananchi wakiendelea kutoa msaada wa kukata miti ili kuokoa Majeruhi .
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi akizungumzia ajali hiyo amesema miili ya waliofariki dunia bado haijatambuliwa pamoja na idadi ya majeruhi.

Amesema waliofariki dunia ni Wanawake watatu na Wanaume wawili ambapo Kati yao yupo mkazi wa Kasharazi aliyekuwa akiendesha baiskeli ambaye basi lilimwangukia.
Mmoja wa mashuhuda Bw. Amiri Salum ambaye ni Dereva aliyekuwa nyuma ya mabasi hayo akitokea Biharamulo, amesema wakati magari yakimalizia mteremko ndipo ajali ilipotokea ambapo yote yalielekea kwenye mashamba ya wakulima


Aidha majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa kwenye hospitali za Murugwanza na Nyamiaga za wilaya ya Ngara kwa ajili ya matibabu zaidi.

Habari/Picha kwa Hisani ya RADIOKWIZERA.CO.TZ

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages