About Me

header ads

AFRIKA ‘IWEKEZE’ KATIKA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA KWA MAENDELEO ENDELEVU

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ambaye pia ni Rais wa Women in Nuclear Tanzania, Profesa Najat Mohammed, akizungumza wakati wa Jukwaa la Wanawake wa Urusi na Afrika kuhusu Nyuklia, amesisitiza umuhimu wa kuwahamasisha wanawake vijana zaidi kufuata taaluma za sayansi na teknolojia ya nyuklia.
-------------------------------------

Na Damas Makangale, Dar es Salaam


Katika nchi nyingi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, teknolojia ya nyuklia mara nyingi kuhusishwa zaidi na vita na nguvu za uharibifu zinazotokana na silaha za nyuklia.


Mtazamo huu umechangia kuwa na uelewa mdogo wa umma kuhusu uwezo wa teknolojia hiyo katika kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.


Hata hivyo, sayansi na teknolojia ya nyuklia zina matumizi mengi zaidi ya masuala ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na huduma za afya, kilimo, maendeleo ya viwanda, utafiti wa kisayansi na uzalishaji wa nishati.


Wakati nchi za Afrika zikichunguza fursa zinazotokana na teknolojia ya nyuklia na rasilimali za urani, wataalamu wanasema kuwa kuongeza uelewa wa umma, uwekezaji katika elimu na maendeleo ya ujuzi ni mambo muhimu katika kuhakikisha bara la Afrika linanufaika kikamilifu na teknolojia hiyo.


Masuala hayo yalijadiliwa kwa kina katika Jukwaa la Wanawake wa Urusi na Afrika kuhusu Nyuklia la mwaka 2026 (Russia–Africa Women’s Nuclear Forum 2026), lililofanyika Dar es Salaam wiki iliyopita, likiwa na kaulimbiu isemayo “Mazungumzo ya Mabara: Nishati ya Nyuklia kwa Mustakabali wa Baadaye.”

Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan, akizungumza wakati wa Jukwaa la Siku Moja la Wanawake wa Urusi na Afrika kuhusu Nyuklia lililofanyika Dar es Salaam wiki iliyopita.

----------------------------

Jukwaa hilo liliandaliwa na Mtandao wa Wanawake katika Sekta ya Nyuklia Tanzania (WiN Tanzania) kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Nyuklia Urusi (Association of Women in Nuclear Russia), kwa msaada wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), WiN Afrika, Shirika la Rosatom, Baraza la Jukwaa la Wanawake la Eurasia na Baraza la Kimataifa la Kusaidia na Kuendeleza Wanawake katika Viwanda na Teknolojia (ICWITI).


Washiriki kutoka Tanzania, Urusi, Misri, Uganda, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia na Afrika Kusini walijadili fursa za kuendeleza sayansi na teknolojia ya nyuklia huku wakihamasisha ushiriki wa wanawake katika sekta hiyo.

Endelea  Kusoma........

Post a Comment

0 Comments