About Me

header ads

DAR CITY, FOX DIVAS WATWAA UBINGWA WA BETPAWA NBL 2025

Timu ya Dar City kwa upande wa wanaume na Fox Divas kwa upande wa wanawake zimetwaa ubingwa wa mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu Tanzania (betPawa NBL 2025) yaliyomalizika Jumamosi kwenye uwanja wa Chinangali, mkoani Dodoma.

Dar City ilitwaa kombe hilo baada ya kuichakaza Kisasa Heroes kwa pointi 80-51 wakati Fox Divas iliisambaratisha timu ya Vijana Queens kwa pointi 65-57.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa timu za Dar City na Fox Divas kutwaa Ubingwa wa ligi ya betPawa NBL.
Kwa mujibu wa rekodi za mashindano hayo, Dar City na Fox Divas kila mmoja zimejizolea zawadi nono kupitia mpango wa Locker Room Bonus (LRB) ya betPawa ambapo kila timu imejishindia Sh20.1 milioni kwa kushinda mechi zote za mashindano hayo.


Post a Comment

0 Comments