Dotto Mwaibale, na Philemon Mazalla-Singida
MUFTI wa Tanzania sheikh Dk.Abubakar
Zubeir leo Septemba 18, 2022 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya
Baraza Kuu la Waislam Mkoa wa Singida
(BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa.
Azungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi alisema
amefurahishwa na ridhishwa na hatua iliyochukuliwa ya kuanzisha ujenzi huo
kwani hayo ndiyo maendeleo yanayotakiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA)
"Mimi na msafara wangu masheikh wote waliofika katika kutekeleza mambo
yetu hapa Singida tumefurahishwa sana na jambo hili na haya ndio mambo yetu ya
bakwata tunayoyazungumza sana kuhusu maendeleo" alisema Mufti Zuberi.
Mufti Zuberi alisema changamoto zote zilizotolewa katika hafla hiyo alisema
baraza na viongozi wapo hivyo wanaona namna ya kuzishughulikia na kuwekana sawa
kwani kila jambo lina taratibu zake namna ya kuzitatua.
Aidha Mufti Zuberi alisema jambolililokubwa ni kwa waislam mkoani hapa
kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awawezeshekufanya mambo yao vizuri na kuondosha
magomvi baina yao.
Taarifa ya ujenzi huo ikitolewa mbele ya Mufti ilieleza kuwa Mwezi Marchi
2022 Sheikh wa Mkoa wa Singida na Baraza la Masheikh waliunda kamati maalumu
ili kuongeza nguvu ya ufuatiliaji wa eneo la ujenzi na kufanikiwa kuipata ndani ya Masjid Taqwa
kwa idhini ya uongozi wa msikiti huo.
Ujenzi wa ofisi hiyo hivi sasa umefikia hatua ya linta kwa gharama ya
Sh.8.2 mILIONI na kaziiliyobakia ni upauaji na umaliziaji ambapo fedha
zilizokadiriwa kumalizia kazi hiyo ni Sh.14 Milioni.
Mufti akiwa njiani kwenda Singida mjini alisimama wilayani Ikungi na kuomba dua kwenye eneo ambalo waislam wa wilaya hiyo wanatarajia kujenga Kituo cha afya na baada ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi la ofisi ya Bakwata alikwenda kutembelea Taasisi ya Majmaul Ahbaab iliyopo eneo la Unyakhindi Manispaaya Singida ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanawake wa kiislam na kutunukiwa Tuzo ya heshima ya Kimataifa na Rais wa Taasisi hiyo Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.
No comments:
Post a Comment