Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Nwaka Mwabulambo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtembelea Bw,Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi na kutoa mchango wa sh. miloni moja kwaajili ya matibabu pia nakumfungulia akaunti ya pamoja (Joint Akauti) kulia ni Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid,Meneja Mikopo wa Benki hiyo Bw. Andrew Chimazi.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
Bi-Fatuma Rashid (katikati) akiushukuru uongozi wa benki
hiyo kwa mchango wao walioutoa (kulia) Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge, na Mkurugenzi wa Hazina wa benki hiyo , Nwaka Mwabulambo.
hiyo kwa mchango wao walioutoa (kulia) Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge, na Mkurugenzi wa Hazina wa benki hiyo , Nwaka Mwabulambo.
Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge (kushoto), akimshuhudia, Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid (katikati) akijaza fomu kwa alama ya kidole kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akaunt) kwa ajili ya michango ya kumsaidia.Uongozi wa benki hiyo ulimtembelea, Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi baada ya kuona matangazo kwenye vyombo vya habari.
Bi-Fatuma Rashid akiwa na mume wake Bw.Salim Rashid ayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
Uongozi wa benki hiyo ukishauriana jambo ulipomtembelea Bw.
Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
........................................................
BENKI ya Biashara ya
Mkombozi imeahidi kuendelea kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa kuchangia
watui wenye mahitaji maalumu.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa benki hiyo kutoa msaada
kwa familia ya Salim Rashid mkazi wa Tuangoma
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam mara baada ya kutembelea familia hiyo Nwaka
Mwabulambo Mkurugenzi wa Hazina wa Benki hiyo alisema kuwa katika kuelekea miaka kumi ya benki hiyo bebki
imeamua kushiriki na familia hiyo kwa kutoa maada wa kuwafungulia akaunti ili
jamii iweze kuwasaidia.
Alisema baada ya kupata taarifa
kutoka katika vyombo mbalimbali kuhusu uhitaji wa Rashid ambaye anasumbuliwa na
saratani uongozi wa benki uliamua kushiriki
kwa vitendo kwa kuisadia familia hiyo
kwa kutoa mchango wa sh. miloni moja sambamba na kufungua akaunti ya pamoja ili
kuirahisishia familia hiyo kwenye zoezi la ukusanyaji wa fedha za msaada kutoka
kwa jamii.
“Kama tunavyofahamu simu za
mkononi zina ukomo wa utoaji fedha hivyo benki kwa kuliona hilo tumeamua kuirahisishia jamii kazi hii kwa
kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akauti) ambayo itawezesha jamii na taasisi
mbalimbali kuchangia kiasi chochote cha fedha ili kuirahisishia
familia hii iweze kupata msaada
wa fedha za matibabu,”alisema Mwabulambo
Alisema kwa kutambua umuhimu wa
kushiriki shughuli za kijamii benki itaendelea kushirikiana na wadau wengine
kuchangia shughukli mbalimbali za kijamii kama njia ya kutoa shukrani kwa kile
wanachokipata kutoka kwa wateja wao ambao ndiyo wadau
Aidha aliongeza kuwa tayari
uongozi wa benki umewashawishi watumishi wake kuona umuhimu wa kuchangia
matibabu ya Rashidi huku ikiwataka watanzania wengine kuona umuhimu wa kutoa
michango kwa familia hii na zinmgine zenye mahitaji .
Aliitaja akaunti namba ambayo
watanzania wanaweza kutoa michango yao kwa familia hiyo kuwa ni 00420111912801 na kusema kuwa kufanya hivyo kutarahisisha matibabu ya Rashid ambaye tayari
alishaanza matibabu hapa nchini na nje
ya nchi.
Kwa upande wake Fatuma Rashid
mke wa Salim Rashid aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa mchango
wao na kuwaomba kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika kufanikisha matibabu
zaidi ya Rashid.
“Nashukuru Benki ya Ukombozi kwa
kuliona tatizo la mume wangu na kulichukulia uzito kwa kuchangia kiasdi hicho
cha fedha sambamba na kufungua akaunti, hii imetupa moyo kuwa jamii ipo pamoja
nasi,”alisema Fatuma.
kufungua akauti kwa familia hiyo ili kuwezesha
jamii kuweza kushiriki kucahngia gharama za matibabu.
“Kama Benki tumeitembelea
familia hii ya Rashid ili kuifariji na
tumeshaifungulia akaunti ya pamoja itakayowezesha jamii kutoa michango yao ya
hali na mali ili kuwezesha matibabu ya Salim ambaye anasumbuliwa na
saratani,”alisema na kuongeza kuwa hii pia itasaidia taasisi mbalimbali kuweza
kuchangia zaidi matibanu hayo.
Hata hivyo aliwaomba watanazia
wote wenye mapenzi mema kuwa karibu na familia hiyo ili kuwezesha matibabu
yaanyike na kuimarisha afya ya mume wake.
No comments:
Post a Comment