About Me

header ads

TAKUKURU SINGIDA YAREJESHA MAGARI YA SHIRIKA LA SEMA YALIYOUZWA KINYEMELA

Gari aina ya Landcruiser VX lililorudishwa Shirika la Sema mkoani Singida

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Singida, Petro Horombe akizungumza Machi 9, 2026 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/ 2026.

............................

Na Dotto Mwaibale, Singida

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na wadau imefanikiwa kurejesha magari manne yaliyokuwa yakimilikiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA) lililopo mkoani Singida.

Magari hayo yalikamatwa na kampuni moja ya udalali kufuatia shirika hilo kushindwa kulipa deni  lililopelekea magari hayo kukamatwa na kampuni hiyo ya udalali na kuyauza kinyume cha sheria.

Pamoja na magari hayo kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 narejeo ya mwaka 2023 TAKUKURU Mkoa wa Singida imefanikiwa kurejesha kiasi cha fedha zaidi ya Sh. Milioni 119.

Hayo yamebainishwa Machi 9, 2026 na  Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Petro Horombe wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/ 2026.

Horombe aliyataja magari hayo kuwa ni Isuzu Tiper  lenye namba za usajili T 423 AED, Landlover 110 lenye namba T412 AED, Isuzu Tiper namba T 418 AED la kubebea vitu vizito pamoja na Landcruizer VX yenye naamba za usajili 465 AED.

Akizungumzia utekelezajı wa ma}ukumu ya TAKUKURU, Horombe alisema  taasisi hiyo imefanıkiwa kusaidia kurejesha zaidi ya Sh. 119 milioni pamoja na magari manne kutokana na kazi za uchunguzi.

“ Chambuzi za mifumo na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo 25 yenye thamani ya Sh. 5,177,915,609.00 katika sekta za Elimu, Maji, Barabara, Afya, na Utawala kiasi hicho cha fedha kilirejeshwa,” alisema Horombe.

Akifafanua zaidi alisema kiasi cha Sh.  S7,585,OOO.00 zilirejeshwa serikalini kutokana na chunguzi za tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wa mali za umma, na magari manne baada ya uchunguzi kwa Taasisi miliki, kutokana  na kuuzwa kinyume cha taratibu.

Horombe aliongeza kuwa Sh. 43,810,000.00 zililipwa kwa wazabuni kwa ajili ya kusambaza vifaa vya ujenzi lakini vifaa hivyo havikufikishwa kwenye maeneo ya miradi na baada ya ufuatiliaji, vifaa vyenye thamani hiyo viliwasilishwa kwenye miradi husika.

Aidha, Horombe alisema Mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi  alijipatia  isivyostahili Sh.7,531,215.00 za kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kutoa Stakabadhi ya kughushi ya EFD baada ya kupokea malipo ya vifaa alivyosambaza kwenye utekelezaji wa mradi wa maendeleo na baada ya ufuatiliaaji, mzabuni huyo aliwasilisha stakabadhi halali ikiwa na makato hayo ya kodi.

Horombe akitoa ufafanuzi zaidi alisema Sh. 2,337,000.00 zililipwa kwa mzabuni baada ya kusambaza vifaa vya ujenzi katika utekelezaji wa mradi visivyo na ubora na sifa zilizotajwa kwenye mkataba na baada ya ufuatiliaji, mzabuni aliwasilisha vifaa stahiki kwa mujibu wa mkataba.

Fedha nyingine zilizorudishwa ni Sh. 2,009,884.63 za ushuru wa huduma zilichukuliwa na wazabuni waliosambaza vłfaa vya ujenzi kwenye miradi ya maendeleo isivyostahili baada ya kutokatwa kwenye malipo yao ambazo zimerejeshwa kwenye akaunti za Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri baada ya uchunguzi.

 Alisema Sh. 1,563,625.25 za kodi ya zuio zilikatwa kwenye malipo ya wazabuni waliosambaza vifaa vya ujenzi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pasipo kuwasilishwa kwenye mamlaka ya Napato Tanzania (TRA) na baada ya ufuatiliaji, fedha hizo ziliwasilishwa TRA kwa mujibu wa sheria.

Horombe aliongeza kuwa Sh. 648,O0O.00 zililipwa ısivyo halali kwa wazabuni waliosambaza vifaa vya ujenzi katika miradi ya maendeleo kwa kuweka gharama kubwa ya vifaa kuliko bei halisi ya soko ambazo zimerejeshwa kwenye akauntı za miradi husika.

Alitaja fedha nyingine zilizorejeshwa ni Sh.  43,810,000.00 ambazo zililipwa kwa wazabuni kwa ajili ya kusambaza vifaa vya ujenzi lakini vifaa hivyo havikufikishwa kwenye maeneo ya miradi naa baada ya ufuatiliaji, vifaa vyenye thamani hiyo viliwasilishwa kwenye miradi husika.

Wakati huo huo Horombe alisema kuwa kupitia uchambuzi wa mfumo wa vyombo vya watumia maji wameweza kurejesha Sh. 3,000,000.00 kwa mwananchi mmoja ambaye alilipa kiasi hicho cha fedha kimakosa kwenye akaunti ya jumuiya ya watumia maji ambapo awali uongozi wa jumuiya hiyo haukuwa tayari kurejesha fedha hizo hadi TAKUKURU ilipoingilia kati.Skauti wakiwa kwenye mkutano huo. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Skaauti Wilaya ya Singida Veronica Mwambije.

Maafisa Usafirishaji wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mary Kalambo,  Mwenyekiti wa madereva na wamiliki wa Bajaji na bodaboda Mkoa wa Singida, Abdul Swalehe na Katibu wa umoja huo Mkoa wa Singida, Abiud Mlowezi.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Senge wakiwa kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.
Gari aina ya Isuzu Tiper linalobeba vitu vizito lililorudishwa na TAKUKURU kwa Shirika la Sema.
Gari aina Isuzu Tiper lililorudishwa Shirika la Sema..
Nyumba iliyorudishwa na TAKUKURU  kwa mmiliki wake.

 

Post a Comment

0 Comments