PIGO JINGINE EFM ,MTANGAZAJI OMARY KATANGA AWAACHIA MANYOYA. - FAHARI NEWS

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, August 8, 2018

PIGO JINGINE EFM ,MTANGAZAJI OMARY KATANGA AWAACHIA MANYOYA.


Hatimaye kitendawili kilichokuwa kinaumiza vichwa vya wasikilizaji na wafuasi wa Efm Redio juu ya ukimya wa muda mrefu wa mtangazaji mahiri Omary Katanga kimepata jibu.

   Sasa ni rasmi mkali huyo wa kipaza sauti katika medani ya michezo ameachana rasmi na Efm redio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni siri nzito iliyopelekea kuchukua uamuzi huo.

  Chanzo cha habari kisicho rasmi  kinaeleza kuwa Katanga a mechoshwa na mambo yaliyokuwa yakimnyima raha na kushindwa kufanya kazi zake kwa uhuru ingawa mambo yenyewe hayajafahamika mpaka sasa.

  Utafiti uliofanywa na (ukurasa huu) umebaini kuwa Katanga maarufu kama 'mlinda mlango' alikuwa akisikiza mara chache kwenye vipindi vya michezo vinavyorushwa na Efm kwa kuanzia na kipindi cha asubuhi ( Sports HQ) na kile cha usiku Esports.

   Kwa wanaofuatilia vipindi hivi mtakubaliana nami kwamba Omary Katanga alikuwa akiendesha kipindi cha Sports HQ mara moja kwa wiki na kile cha usiku akisikika mara tatu tu jambo lililozua maswali kwa wadau wa michezo pamoja na mashabiki wake.

   Baadhi ya wadau tuliozungumza nao walikuwa na mitazamo tofauti,wengine wakisema ukimya wa Katanga umesababishwa na majukumu mengi aliyonayo kwakuwa alikuwa pia ni miongoni mwa wasomaji mahiri wa taarifa za habari.

   Huku wengine wakidai kwamba style na uwezo alionao Katanga  wa kutawala kipaza sauti awapo studio huenda vimewatisha wakongwe waliopo pale ambao bila ubishi wowote wanaendelea kupoteza mvuto ( hawana jipya).

  Mtangazaji Omary Katanga anayekubalika na wengi kutokana na umahiri wake wa kutawala kipaza sauti awapo studio,alijiunga na Efm tangu mwaka 2014 akitokea Redio One.

  Wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi nyota huyo ataelekea kuendeleza cheche zake baada ya kuachana na Efm? Tusubiri tuone,lakini juhudi za kupata ufafanuzi wa taarifa hizi kutoka kwa Katanga mwenyewe zimegonga mwamba kwakuwa anadai hayupo tayari kulizungumzia suala hilo kwa sasa.

  Hata hivyo tumejaribu pia kumtafuta rafiki yake wa karibu anayefahamika kwa jina la Master Tindwa,lakini akasema kuwa yeye pia amezisikia juu juu taarifa hizo na kwamba si msemaji.

"Ni kweli Katanga ni rafiki yangu mkubwa,lakini hilo halinifanyi kuwa msemaji wake,yeye mwenyewe muhusika ndiyo ana nafasi nzuri ya kulizungumzia suala  hilo" Alisema Tindwa.

  Tunawaahidi wasomaji wetu kwamba tutaendelea kuzifuatilia taarifa hizi na kuwajulisha kinachoendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages