Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuwa akimunesha
mpaka wa kijiji hicho na Pori la Akiba Mkungunero wakati wa ziara yake
ya kikazi katika pori hilo jana Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili
ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji
jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa
kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta
suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Na Hamza Temba - Kondoa, Dodoma
....
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7 februari,
2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya Kondoa Mkoani
Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo kusubiri uamuzi wa
Serikali utakaoshirikisha Wizara yake, Wizara ya Ardhi na Tamisemi
katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya ardhi katika pori
hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu.
Dk.
Kigwangalla ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alitembelea
vijiji vinne vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko na kufanya
mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujiridhisha na kujifunza juu ya
mgogoro uliopo baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero.
"Nimefika
hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi lakini
pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba niende
nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na mwisho
wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na changamoto
ambazo zimekuwepo.
"Niwaombe
sana wakati Serikali inaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro huu ni vema
tukafuata sheria zilizopo, tuzingatie mipaka iliyowekwa ili tusiingie
kwenye migogoro, lakini kwa sasa siwezi kwa namna yeyote ile kutamka
neno la kujibu maombi ya mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na wananchi
yaliyotolewa hapa leo.
"Kama
Serikali tutakaa, Wizara yangu, Wizara ya Ardhi na Tamisemi ili tujue
kiini cha mgogoro huu tufanye uamuzi kuwa ni maeneo gani yaongezwe
katika hifadhi kwa ajili ya wananchi au ni vitongoji vipi vifutwe,
tutaleta majibu, na jambo hili tutalifanya kwa uadilifu mkubwa bila
kumuonea mtu ili kumaliza mgogoro huu," alisisitiza Dk. Kigwangalla.
Awali
akimkaribisha Waziri huyo kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ikengwa,
Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Ashatu Kijaji alisema kutokana na ukweli kuwa
Serikali ya awamu ya tano inasikiliza kero za wananchi na kuzipatia
ufumbuzi, ni vema Waziri huyo akatumia hekima na kuangalia uwezekano wa
kuwapa wananchi hao Kilomita 12 za mraba kutoka kwenye hifadhi hiyo kwa
ajili ya kuendesha shughuli zao za kibinadamu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi alisema
mgogoro baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero ulinza mwaka
2006 kufuatia zoezi la kuanzishwa kwake pamoja na lile na uwekagi wa
vigingi vya mpaka na vijiji jirani kutoshirikisha wananchi na viongozi
wa halmashauri za vijiji hoja ambayo ilipigwa na Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso.
Aidha
alisema wananchi wa vijiji hivyo wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya
kilimo na ufugaji, hivyo akamuomba Waziri huyo pamoja na Serikali kwa
ujumla kutumia busara kuwamegea wananchi wa vijiji hivyo eneo la
Kilomita 12 za mraba kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.
Naye
Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso alisema Pori la Akiba Mkungunero
lilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 307 la mwaka 1996 baada ya
kupandishwa hadhi kutoka Pori Tengefu. Alisema mchakato wa kupandisha
hadhi pori hilo ulishirikisha wananchi na viongozi wa vijiji na wilaya
ambapo mihutasari mbalimbali ilisainiwa.
Alisema
pori hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazochochea mgororo
huo ikiwemo kijiji kimoja cha Kisondoko kusajiliwa kimakosa ndani ya
hifadhi hiyo pamoja na malalamiko mbalimbali ya wananchi kuwa
hawakushirikishwa kwenye uanzishwaji wa pori pamoja na madai mengine
kuwa pori hilo limeingilia mipaka ya vijiji hivyo.
Pori
la Akiba Mkungunero ambalo lina ukubwa wa Kilimita za Mraba 557.9 lina
umuhimu mkubwa kiuchumi na kiikolojia kwa kuwa ni chanzo muhimu cha mto
Tarangire ambao ni uhai wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire na ikolojia
nzima ya ziwa Manyara. Pori hilo pia ni sehemu ya mapito na mazalia ya
wanyamapori pamoja na makazi ya wanyamapori adimu duniani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kondoa muda mfupi baada ya
kuwasili wilayana humo jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya
Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori
hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto
za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia
ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro
huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya
Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori
hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto
za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia
ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro
huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteja
jambo na Meneja wa Pori la Akiba Mkungunero, Emannuel Bilaso wakati wa
ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa
Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta
jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi wakati wa
ziara yake ya kikazi jana katika Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya
Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa
mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa
kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na
TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea mabango ya
malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisondoko kuhusu Pori la
Akiba Mkungunero na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kikazi katika
pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko wilayani Kondoa jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya
Pori la Akiba Mkungunero na mmoja wa wahifadhi wa Pori hilo wakati wa
ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa
Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori
hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema
Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa
pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la
Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Ashatu Kijaji.
No comments:
Post a Comment