Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga (kulia) akifungua kikao
cha Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni
kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi
kibiashara, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina .
( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, Enock
Balilemwa akizungumza kwenye kikao cha
cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori
hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa
lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha
wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo
Mwina akizungumza kabla ya kumkaribisha
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kufungua kikao
cha Wawakilishi wa
Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai
kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa
lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha
wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
(
Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, Fatuma Hamisi
akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
(hayupo pichani) kwenye kikao cha cha
Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori
hai kilichofanyika jana mjini Dodoma ikiwa
lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha
wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
( Picha na Lusungu Helela-MNRT
Baadhi ya Wawakilishi
wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma kati
ya Wizara na wadau hao lengo likiwa ni
kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi
kibiashara.
( Picha na Lusungu
Helela-MNRT)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga na
Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni
kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi
kibiashara.
( Picha na Lusungu
Helela-MNRT
Mjumbe wa Halmashauri wa TWEA, Paul Madinda ambaye pia ni mmiliki wa shamba la viumbe hai jijini Arusha, akizungumza mbele ya Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani) jinsi
alivyoathirika tangu zuio hilo la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi
lilipotelewa kwenye kikao cha cha
Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori
hai kilichofanyika jana mjini Dodoma.
(
Picha na Lusungu Helela-MNRT
Chama
cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya
nchi kibiashara (TWEA) kimeiomba
serikali isitishe zuio la kusafirisha nje wanyamapori hao ili wanachama
wake waweze kujikwamua na hali ngumu ya
maisha inayaowakabili.
Wakizungumza
mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga kwenye
kikao cha Wizara na wawakilishi wa Wafanyabiashara hao waliiomba serikali
isikilize kilio chao.
Kwa
upande wake , Mwenyekiti wa Chama hicho, Enock Balilemwa alisema baadhi ya wanachama wakiwemo
walemavu waliokuwa wamechukua mikopo benki wamefukuzwa kwenye nyumba zao baada ya
kushindwa kufanya marejesho ya mikopo hiyo kufuatia zuio la biashara hiyo.
Alieleza
kuwa baadhi ya wanachama wake wamejikuta
kwenye hali ngumu ya kupoteza mali zao na kuingia kwenye mifarakano na wateja
wao kwa vile wafanyabiashara hao walichukua
pesa toka kwa wateja kama malipo ya
awali hivyo wakati wa zoezi la kusimamisha biashara linafanyika liliwakuta
wafanyabiashara hao wameshachukua pesa za wateja wao kama malipo ya awali.
Naye,
Makamu Mwenyekiti wa TWEA, Fatuma Hamis alimweleza Naibu Waziri kuwa zuio hilo lilifanywa ghafla mno bila kutoa
muda kwa wafanyabiashara hao ukizingatia kuwa walikuwa wakimiliki leseni halali
walizokuwa wamezilipia pesa bila kuzifanyia kazi ya kuwaingizia kipato.
Aidha,
alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa zuio
hilo limepelekea wafanyabiashara hao kupoteza uaminifu kwa wateja wao na
kuwaweka kwenye mazingira magumu ya ushindani kibishara kwani biashara hiyo
haifanywi na Tanzania pekee.
Wakati
akijibu hoja za Wafanyabiashara hao, Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara (TWEA)
,kuyafanyia kazi malalamiko yao kadri itakavyowezekana na kuja na kauli moja ya
serikali.
Amesema
lengo la serikali la kuzuia usafirishaji wanyamapori hao lilikuja baada ya
wafanyabishara ambao sio waaminifu kukengeuka kwa kuanza kujihusisha na
ujangili pamoja na kusafirisha wanyamapori ambao hawamo kwenye orodha ya vibali
walivyopewa.
‘’Dhumuni
la serikali la kusitisha biashara hii
ilikuwa ni njema tu baada ya
kuona wajanja wachache wananufaika huku wanyonge wakibaki watazamaji kwenye
rasilimali zao’’ alisema Hasunga
Hata
hivyo, Naibu Waziri Hasunga alisema
lengo la serikali halikulenga kuwakomoa
bali ni kutaka kuweka mfumo mzuri utakaomsaidia kila Mtanzania aone ananufaika na rasilimali za
nchi yake.
‘’Nimewasikiliza
kwa umakini wa hali ya juu lakini hata hivyo Serikali ina utaratibu wake wa
kutoa majibu, tupeni muda ili tukitoa majibu kuhusu hoja zenu kuwe na jibu moja
kwa kila mmoja wetu’’ alisema
Katika
hatua nyingine, Hasunga aliwataka wafanyabishara hao wasisite kuonana nae muda wowote ule kwa kumpigia simu au kwa kuonana nae pindi
wanapokuwa na jambo la kutaka kuzungumza nae kwa ajili ya manufaa mapana ya
Wizara na nchi kwa ujumla.
Naye,
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina aliwahakikishia wafanyabiashara kufanyia kazi
malalamiko yao kutokana na hoja za
msingi zilizowasilishwa na
wafanyabiashara hao.
‘’Nimesikia
baadhi ya malalamiko yenu ambayo kwa nafasi yangu niliyo nayo kwa kushirikiana
na watumishi walio chini yangu nitayashughulikia’’ alisema.
No comments:
Post a Comment