About Me

header ads

WATU WENYE ULEMAVU JIMBO LA MTUMBA KUWEZESHWA NA MIRADI YA KIUCHUMI

▪️Rais Samia apongezwa kwa kuwajali na kuwathamini watu wenye ulemavu

▪️Mbunge Mavunde aahidi miradi ya uchumi kwa watu wenye ulemavu

▪️Agawa vifaa vya usaidizi na sadaka ya sikukuu

▪️SHIVYWATA Dodoma waishukuru Serikali kwa utatuzi wa changamoto zao


Mbunge wa Jimbo la Mtumba na Waziri wa Madini,  Mh. Anthony Mavunde akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya usaidizi kwa watu wenye ulemavu wa Jimbo la Mtumba Aprili 4, 2026.

......................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WANANCHI wenye ulemav Jimbo la Mtumba Mkoa wa Dodoma kupitia programu mbalimbali za uwezeshwaji wananchi kiuchumi na mikopo ya Serikali kuwezeshwa miradi ya kiuchumi ili waweze kujitegemea na kujiendeleza kiuchumi.

Hayo yamesemwa Aprili 4, 2026 na Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya usaidizi kwa watu wenye ulemavu wa Jimbo la Mtumba.

“Tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuwajali na kuwaendeleza watu wenye ulemavu nchini.

Suala la mikopo na uwezeshwaji kiuchumi watu wenye ulemavu ni ukombozi mkubwa katika kuwafanya waweze kujitegemea.

Jimbo la Mtumba tumeandaa programu mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi”alisema Mavunde

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu(SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma . Omar Lubuva ameishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za watu wenye ulemavu,pia amemshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada wa viti mwendo na fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa hiyo ni hatua kubwa katika kupunguza changamoto za watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi amesema serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na watu wenye ulemavu katika utatuzi wa changamoto zao pamoja na kuendelea kuongeza fursa za kiuchumi kwa kundi hili.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma . Omar Lubuva akiteta jambo na Mbunge wa Mtumba Mhe. Mavunde wakati wa hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma . Omar Lubuva, akizungumza kwenye hafla hiyo. 
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi akizungumza kwenye haafla hiyo.
Mbunge wa Mtumba Mhe. Mavunde akizungumza na mmoja wa watu wenye ulemavu wakati wa hafla hiyo.
Taswira ya hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.

Mbunge wa Mtumba Mhe. Mavunde akimfariji mmoja wa watu wenye ulemavu aliyekuwa akilia kwa furaha ya kukabidhiwa kiti mwendo wakati wa hafla hiyo.

Hafla hiyo ikifanyika
Mama mwenye uoni hafifu akimshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada aliowapa.

Mbunge wa Mtumba Mhe. Mavunde  akimkabidhi fimbo nyeupe mmoja wa wananchi aliyefika kwenye hafla hiyo.

Post a Comment

0 Comments